Visa 61 viliripotiwa, ikiwa ni mara mbili ya ilivyorekodiwa miaka mitano iliyopita.
Watu 103 waliuawa na 140 kujeruhiwa mwaka 2021. Hesabu hiyo haijumulishi watu waliokuwa wakitekeleza mashambulizi hayo.
Ripoti hiyo imetolewa siku 9 baada ya kijana mwenye umri wa miaka 19 kuwaua watu 10 na kujeruhi wengine watatu katika jamii inayokaliwa sana na watu weusi, katika mtaa wa Buffalo, mjini New York.
FBI inachunguza kisa hicho kama cha uhalifu wa chuki na kilichochochewa na ubaguzi wa rangi.