Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:26

Visa vya COVID-19 Kenya vinaongezeka katika majimbo ya mpakani


Mfanyakazi wa huduma ya afya akionesha mfuko wenye sampuli za COVID-19 katika moja ya kaunti za Kenya. April 22, 2020.
Mfanyakazi wa huduma ya afya akionesha mfuko wenye sampuli za COVID-19 katika moja ya kaunti za Kenya. April 22, 2020.

Visa vya maambukizi ya Corona nchini kenya  vimefikia watu 10,105 huku majimbo yaliopo mipakani mwa taifa hilo la Afrika mashariki yakishuhudia kupata virusi hivyo kutoka mataifa jirani

Serikali ya kenya inasisitiza watu kutilia mkazo maagizo ya afya ili kuzuia maambukizi kusambaa katika jamii zinazoishi mipakani.

Kwa mujibu wa wizara ya afya Kenya majimbo matatu ikiwemo Kajiado, Busia na Kwale japo visa hivyo vinathibitishwa lakini bado kuna changamoto. Kati ya mikakati kwenye mipaka hiyo ni kuhakikisha madereva wa malori ya mizigo na matrela wanapimwa kabla ya kuruhusiwa kuingia kenya.

Katika kaunti ya Kwale ambayo inaunganisha nchi ya kenya na Tanzania kwenye mpaka wa Lungalunga kati ya visa 139 ambavyo vimeripotiwa tangu mwezi Marchi, visa 80 ni raia wa Tanzania na Malawi. Anaeleza Salim Mvurya, Gavana wa jimbo la Kwale.

Haya yanajiri baada ya muafaka uliopatikana kati ya Kenya na Tanzania mapema mwezi Juni, wakati ambapo msongamano wa malori ulishuhudiwa mpakani huku kila nchi ikimnyooshea mwenzake kidole cha lawama.

Mercy Mwangangi, naibu katibu katika wizara ya afya akiwa ziarani pwani ya Kenya mwishoni mwa wikiendi alidokeza kuwa hakuna msongamano wa malori unaoshuhudiwa kwa wakati huu.

Alisema Serikali inatumia mabalozi wa nyumba kumi pamoja na raia katika kuwafichua raia wa Tanzania na wakenya wanaotumia njia za vichochoroni kuingia ndani ya taifa jingine.

Naye kaimu mkurugenzi wa afya kenya, Dr. Partric Amoth, alisema kuwa mikakati ya mipakani imesaidia kudhibiti maambukizi kusambaa kwenda jamii zinazoishi karibu. “mikakati tunayoifanya imezaa matunda ndio maana hakuna visa vilivyoripotiwa katika jamii maana haviwafikii. Tunaomba Ugonjwa huu umalizike na baada ya corona kuisha vifaa vilivyoko vitasaidia wengine”.

Haya yanajiri huku Kenya ikiripoti visa 10,105 kufikia siku ya Jumapili na wakati huo huo wahudumu watatu wa afya walifariki kutokana na maambukizi ya Corona huku wakiwa katika mazingira ya kazi.

Amina Chombo, VOA Mombasa

XS
SM
MD
LG