Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:55

Wamarekani washeherekea sikukuu ya 'Thanks Giving'


Maandamano ya sikukuu ya Thanks Giving New York Marekani, Novemba 22, 2018.
Maandamano ya sikukuu ya Thanks Giving New York Marekani, Novemba 22, 2018.

Wamarekani Alhamisi wanasherehekea sikukuu kubwa ya mwaka ya kutoa shukrani kwa mafanikio ya mwaka mzima inayo julikana kama 'Thanks giving day', siku ambayo familia hukutana pamoja kwa mloo wa kitamaduni wenye kitoweo cha bata mzinga.

Huu ni utamaduni ulioanzishwa tangu walowezi wa kwanza kutoka ulaya walipowasili hapa Marekani na kusherehekea mavuno ya kwanza katika karne ya 17 na kusheherekea Alhamisi ya tatu ya mwezi wa Novemba.

Huu ni wakati ambapo Wamarekani husafiri kuelekea nyumbani kuonana na familia na marafiki zao, na chama cha waendesha magari cha triple AAA kinaeleza kwamba huu ni mwaka ambao kutakuwa na idadi kubwa ya wasafiri kwa ndege, treni na magari katika kipindi cha miaka 10 kutokana na hali nzuri ya kiuchumi.

Inaripotiwa kwamba karibu watu milioni 51 watasafiri kwa zaidi ya km 80, hiyo ikiwa ongezeko la asilimia 3.3 kuliko mwaka jana.

Hiki pia ni kipindi cha ukarimu pale Wamarekani wenye uwezo pamoja na mashirika na miji mbali mbali huwasaidia wenzao ambao hawana uwezo kwa kuwapatia chakula ili waweze pia kusherehekea.

Na siku ya pili tu baada ya Thanksgiving Wamarekani humiminika madukani kuanza kununua zawadi za sherehe za mwisho wa mwaka, siku inayofahamika kama Black Friday, ambapo maduka ya biashara hupunguza bei za bidhaa zao kwa hadi asilimia 60.

Siku hii ya kutoa shukurani kwa mwenyezimungu hufanyika pia Canada, nchi za Amerika ya Kati na baadhi ya waumini wa Kikristo huwenda kanisani kwa misaa maalum ya siku kuu hii.

Kwa upande wa kidini thanksgiving kulingana na wanahistoria ilianzishwa wakati wa enzi ya mfalme Henry wa nane wa Uingereza mnamo mwaka 1536.

XS
SM
MD
LG