Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 01:01

Viongozi Tanzania waahidi kuimarisha uhusiano na China


Dkt. Mwakyembe
Dkt. Mwakyembe

Viongozi mbalimbali nchini Tanzania wameungana pamoja kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China.

Viongozi hao waliyasema hayo Dar es Salaam jana katika hafla ya kumuaga Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youging, wakisisitiza kuimarisha uhusiano huo kati ya mataifa hayo mawili, vyanzo vya habari vimesema nchini Tanzania.

Akizungumza, Dkt Mwakyembe amesema China imekuwa rafiki wa kweli kwa kusaidia uboreshaji wa sekta mbalimbali zikiwemo za habari, utamaduni, sanaa, michezo, lakini pia viwanda, mawasiliano, uchukuzi, afya na elimu kwa uwezo wa juu zaidi.

“Kwa mfano katika wizara yangu ya sasa Machi mwaka huu, serikali za Tanzania na China zilitia saini mkataba wa ushirikiano wa utamaduni wa miaka mitatu ambapo vijana 200 wa Tanzania watakwenda China kila mwaka ili kusoma masuala ya habari, sanaa, utamaduni.

“Huu ni ushahidi wa ushirikiano wa kiwango cha juu sana ambao ulianza tangu wakati wa waasisi wetu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Tse-Tung wa China ambao umenogeshwa zaidi sasa na Rais wetu John Magufuli na Rais Xi Jinping ambao wamesogeza sana uhusiano huu kuwa wa karibu zaidi,” alisema Dk Mwakyembe.

Kwa upande wake, Balozi Dk Salim amesema msaada wa China kwa Tanzania, hauwezi kuishi kupimwa katika mtazamo wa kiuchumi tu, bali pia katika ukombozi wa Bara la Afrika kupitia msaada wa ujenzi wa reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) iliyogeuka kuwa kichocheo kikubwa cha ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

Aliongeza kuwa wananchi wa China walikubali kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa reli hiyo huku wakikabiliwa na ufukara wao na serikali yao na wameendelea kuwa marafiki wa kweli kwa Watanzania bila kuwageuka, hadi Taifa hilo lilipofanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuwa moja ya nchi tajiri duniani.

Kwa upande wake, Balozi Lusinde amesema umuhimu wa uhusiano wa Tanzania na China, umeegemea zaidi katika sababu za kihistoria kutokana na watu wa nchi zote mbili kujitoa kwa ajili ya wenzao, akitolea mfano namna Mwalimu Nyerere akishirikiana na Dk Salim walivyofanikisha kuifanya China kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG