Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:46

Sudan Kusini yataka iundwe tume ya ukweli


Viongozi wa Sudan Kusini ambao walikubaliana na kuunda serikali ya pamoja hivi karibuni, wametaka iundwe tume ya ukweli kama ilivyokuwa nchini Afrika ya Kusini ili kuponya vidonda sugu vilivyotokana na vita vikali katika nchi hiyo iliyo changa zaidi ulimwenguni.

Rais Salva Kiir na Makamu wake aliyeteuliwa hivi karibuni, Riek Machar, na ambaye alikuwa hasimu wake wa kisiasa, wameandika taarifa kwenye gazeti la 'New York Times' na kutoa hakikisho kwamba Sudan Kusini haitaingia tena kwenye machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Viongozi hao wawili wamesema kuwa wangetaka kuunda tume ya ukweli na maridhiano inayofanana na ile iliyoundwa nchini Afrika Kusini au Ireland Kaskazini. Taarifa hiyo ilionekana kutupilia mbali uwezekano wa kuwaadhibu waliotekeleza maovu katika siku zilizopita.

Wamesema kutafuta haki kwa njia ya kusdhibu, hata kama kutafanywa katika misingi ya sheria za kimataifa, kutaathiri juhudi za kuliunganisha taifa na kufufua tena hasira na uhasama baina ya wananchi wa Sudan Kusini.

XS
SM
MD
LG