Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 14:44

Viongozi wa Rasi ya Korea wakubaliana kuondosha silaha za nyuklia


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akiwa na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in

Mkutano wa kihistoria baina ya Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in umeanza Ijumaa kaitka kijiji cha truce village huko Panmunjom.

Kim Jong-un alivuka eneo la mpakani lisilokuwa na harakati za kijeshi ambalo limeyagawanya mataifa hayo mawili kwa zaidi ya miaka 60.

Hatimaye viongozi hao kutoka upande wa utawala wa kikomunisti (kaskazini) na upande wa utawala wa kidemokrasia (kusini) walikaribiana kabla ya kutangaza azma yao ya kuondoa silaha za nyuklia na kuendeleza amani.

“Leo, Mwenyikiti Kim Jong Un na mimi tumethibitisha ile azma yetu ya kufikia hali ya kutokuwepo silaha za nyuklia katika eneo la rasi ya Korea katika hatua ya kuondosha kabisa silaha za nyuklia ikiwa ni lengo letu la pamoja,” amesema Rais Moon Jae katika sherehe za kutangaza makubaliano ambayo wameyaita tamko la Panmunjom.

Kiongozi wa Korea Kaskazini kwa upande wake amesema kuwa amekubaliana na Tangazo hilo la pamoja na mikataba iliyotangulia baina ya nchi hizo mbili bila ya kufafanua au kuthibitisha matokeo ya makubaliano hayo ya kuondosha vitisho vya programu ya silaha za nyuklia za nchi hiyo

“Tumeamua kufungua awamu hii ya kuboresha mahusiano na maendeleo kwa kutekeleza kikamilifu Tangazo la Kaskazini- Kusini na mikataba yote iliyotangulia ambayo ilikubalika.,” amesema Kim.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG