Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 10:31

Viongozi wa mapinduzi Niger wasema waendelea kusubiri jibu kutoka ECOWAS

FILE PHOTO: Jenerali Abdourahmane Tiani, aliyetangazwa kuwa kiongozi mpya wa Niger na wanajeshi waliofanya mapinduzi alipokutana na mawaziri huko Niamey.
FILE PHOTO: Jenerali Abdourahmane Tiani, aliyetangazwa kuwa kiongozi mpya wa Niger na wanajeshi waliofanya mapinduzi alipokutana na mawaziri huko Niamey.

Niger Jumatatu imekuwa ikisubiri jibu kutoka Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi baada ya viongozi wa mapinduzi kupuuza siku ya mwisho iliyowekwa kumrejesha madarakani rais aliyeondolewa.

Kitendo cha kupuuzia kutekeleza hatua hiyo imepelekea ECOWAS kuonya kuwa inaweza kusababisha uingiliaji kati wa kijeshi.

ECOWAS, imesema itatoa taarifa kwa hatua zinazofuata, kuujibu utawala wa kijeshi kukataa kutekeleza maagizo ifikapo Jumapili iliyopita, kama nchi za kigeni zenye nguvu zinavyosema zinatarajia kuwepo na suluhu ya amani.

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS baada ya mkutano wao mjini Abuja, Nigeria, Jumapili, Julai 30, 2023.
Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS baada ya mkutano wao mjini Abuja, Nigeria, Jumapili, Julai 30, 2023.

ECOWAS imechukua msimamo mgumu wakati wa mapinduzi yaliyofanyika Julai 26 ikiwa ni ya saba katika eneo hilo katika kipindi cha miaka mitatu.

Licha ya kwamba nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa uranium na mafuta na nafasi yake katika vita vya wanamgambo wenye msimamo mkali wa kiislamu, Niger inashikilia nafasi muhimu ya kimkakati kwa ajili ya Marekani, Ulaya, China na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG