Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:20

Viongozi wa kikurdi wanaripoti kuwepo mafanikio huko Iraq


Mwanajeshi wa kikosi maalum huko Iraq kinachopambana na IS
Mwanajeshi wa kikosi maalum huko Iraq kinachopambana na IS

Viongozi wa kikurdi wanaripoti mafanikio ya mapema wakati wanajeshi wa Irak wakianzisha mashambulizi ya nchi kavu ili kuuteka tena mji wa Mosul uliopo kaskazini mwa Irak kutoka kundi la wanamgambo wa Islamic State.

Rais wa wakurdi, Masoud Barzani alisema katika mkutano na waandishi wa habari hapo Jumatatu kwamba ardhi yenye ukubwa wa kilomita 200 za mraba imekombolewa katika siku ya kwanza tangu operesheni hiyo kuanza. Mji wa Mosul utakuwa huru, Barzani alisema akiongeza kwamba wapiganaji wake wanafanya vyema ili kuukomboa mji wa Mosul na kuhakikisha hautakua kama mji wa Aleppo, akifananisha na mji huo uliokumbwa na vita huko Syria.

Wakati huo huo wakuu wa Pentagon wakieleza mafanikio yanayopatikana kabla ya muda waliopanga wakisema kwamba matokeo yake yanaweza kua na athari kubwa kwa mkakati wa Marekani katika kanda nzima.

Hii ni operesheni kubwa ya kijeshi kufanyika Irak tangu vikosi vya mapigano vya Marekani vilipoondoka miaka mitano iliyopita lakini inaongeza wasi wasi kuhusu usalama wa maelfu ya raia katika eneo.

XS
SM
MD
LG