Nchi hiyo ambayo ni moja kati ya nchi maskini duniani, inategemea sana msaada wa kigeni kusaidia wanainchi wake milioni 25, lakini msaada huo ulipungua tangu wanajeshi walipomuondoa madarakani rais Mohamed Bazoum tarehe 26 Julai.
“Niger inakabiliwa na vikazo vikali vilivyowekwa na mashirika ya kimataifa na kikanda. Vilisababisha mapato kupungua sana,” viongozi wa kijeshi walisema kwenye televisheni ya taifa Ijumaa jioni.
Bajeti ya mwaka wa 2023 ilipunguzwa kwa asilimia 40 hadi dola bilioni 3.2, taarifa hiyo imesema.
Forum