Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:53

Viongozi wa kijeshi Guinea kuunda serikali ya mpito


Kiongozi wa mapinduzi ya Guinea Kanali Doumbouya,
Kiongozi wa mapinduzi ya Guinea Kanali Doumbouya,

Viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea Jumatatu wameahidi kuunda serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa baada ya kumuondoa madarakani Rais Alpha Conde, na kuvunja baraza lake la mawaziri.

Mapinduzi ya Jumapili ambapo Conde na wanasiasa wengine wa ngazi ya juu walikamatwa na kuzuiliwa kusafiri, ni ya tatu tangu mwezi Aprili katika eneo la Afrika magharibi na ya kati, na kuzusha wasiwasi wa kurejea tena uongozi wa kijeshi katika eneo hilo ambalo lilikuwa limepiga hatua kwenye demokrasia ya mfumo wa vyama vingi tangu mwaka wa 1990.

Mapinduzi hayo ya kijeshi yalilaaniwa na jumuia ya kimataifa ambayo inaweka shinikizo kwa viongozi wapya wa kijeshi kueleza mipango yao baada ya kumuondoa Conde, na kuwahakikishia wawekezaji kwamba mauzo ya nje ya bidhaa muhimu za nchi hayatasitishwa.

“Mashauriano yatafanyika kufafanua mfumo mzima wa mpito, kisha serikali ya umoja itaundwa kuongoza mpito,” kiongozi wa mapinduzi Mamady Doumbouya ameambia mkutano wa baraza la mawaziri la Conde na maafisa waandamizi wa serikali.

Ameongeza kuwa “ Mwisho wa kipindi cha mpito, watajikita kwenye enzi mpya ya utawala na maendeleo ya uchumi”.

Doumbouya hakusema uongozi wa mpito utawashirikisha akina nani na kutoa tarehe ya kurudi kwenye uchaguzi wa kidemokrasia.

XS
SM
MD
LG