Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 10:59

Viongozi wa kidini Tanzania waonya dhidi ya utumiaji nguvu na polisi


Freeman Mbowe kiongozi wa CHADEMA akifikishwa mahakamani Arusha
Freeman Mbowe kiongozi wa CHADEMA akifikishwa mahakamani Arusha

watu watowa maoni yanayotafautiana juu ya mustakbal wa kisiasa Tanzania wakati huu ambapo kuna vuguvugu la migogoro baina ya wanasiasa, wananchi na vyombo vya dola.

Viongozi wa dini kupitia Jumuia ya Kikristo Tanzania-CCT wameitaka serikali kutofanyia mzaha vuguvugu za kisiasa zinazoendelea hivi sasa nchini humo, wakiashiria kwamba ni chanzo cha kupoteza amani nchini Tanzania.

Onyo hilo linatolewa wakati kiongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, kuachiwa kwa dhamana Jumatatu mjini Arusha.

Hakimu mkuu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Arusha Charles Magesa, ameondoa hati ya kukamatwa mwenyekiti huyo wa taifa wa CHADEMA baada ya kufikishwa kizimbani.

Kiongozi huyo alifikishwa mahakamani Arusha akitokea Dar es Salaam ambako alikamatwa na polisi na kuwekwa rumande kwa siku mbili kabla ya kusafirishwa kwa ndege ya jeshi saa tisa usiku chini ya ulinzi mkali.

Mbowe ambaye pia ni mkuu wa kambi ya upinzani bungeni aliwekwa rumande Jumamosi baada ya kujisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha kati cha polisi jijini Dar Es Salaam baada ya mahakama ya Arusha kutoa amri akamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana ya kutofika mahakamani hapo kusikiliza kesi iliyokua ikimkabili wiki iliyopita.

Habari zaidi zinasema kwamba pamoja na kuwepo kwa ulinzi mkali na umati mkubwa wa watu mahakamani hapo hakuna ghasia ya aina yeyote iliyotokea na kesi hiyo imeahirishwa mpaka Juni 24 mwaka huu.

Mbowe na wenzake wanatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali katika maandamano ya chama hicho yaliyofanyika mjini Arusha Januari tano mwaka huu, kupinga uchaguzi wa meya wa jiji hilo la Arusha.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Erasto Tembo, mkurugenzi wa habarina uwenezi wa CHADEMA, anasema wanasikitishwa na jinsi polisi walivyomtendea kiongozi wao ambae ni mbunge na ana kinga kutokana na malalamiko madogo kama hayo.

XS
SM
MD
LG