Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:48

Viongozi wa juu Marekani watarajia kufikia muafaka


Seneta Harry Reid akiwa nje ya jengo la bunge katika mashauriano ya kufungua tena serikali kuu ya Marekani
Seneta Harry Reid akiwa nje ya jengo la bunge katika mashauriano ya kufungua tena serikali kuu ya Marekani
Kiongozi wa walio wengi katika baraza la Seneti m-Democrat Harry Reid anasema anamatumaini kutakuwa na matokeo mazuri katika juhudi za kufungua tena serikali kuu na kuongeza kiwango cha kukopa.

Reid alizungumza kwenye jukwaa la Seneti katika kikao cha faragha kilichofanyika Jumapili. Reid alisema yeye na kiongozi wa Repuplican Mich McConnell walikuwa na mazungumzo muafaka lakini hakufafanua zaidi.

Awali Reid aliwakosoa wa-Republican katika baraza la Seneti ambao walikataa mpango wa Democrat wa kuongeza udhibiti wa kiwango cha serikali cha kukopa hadi mwaka ujao. Warepuplican bungeni wanapendekeza ongezeko la muda mfupi na wanataka ongezeko lolote lijumuishe kupunguza matumizi.

Christine Lagarde
Christine Lagarde

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la fedha-IMF Christine Lagarde alikiambia kituo cha televisheni cha NBC katika kipindi cha Meet the Press siku ya Jumapili kwamba kushindwa kuongeza kiwango cha kukopa itamaanisha kwamba kutatokea uharibifu mkubwa duniani na itaweza kuongeza hatari nyingine ya kudorora kwa uchumi ulimwenguni.

Kiwango cha kukopa cha hivi sasa kinaisha Alhamis. Kama bunge halitaongeza kiwango hicho Marekani haitaweza tena kukopa fedha na kuwalipa wadeni wake au kukidhi majukumu mengine.

Pia kufungwa kwa baadhi ya ofisi za serikali kuu kunaanza wiki yake ya tatu siku ya Jumanne kukiwa hakuna dalili za mafanikio kati ya bunge na White House. Reid alisema wiki iliyopita kwamba kufungwa kwa serikali kuu kunasababisha maumivu na mahangaiko nchi nzima.

Rais Barack Obama na wa-Democrat wanalitaka bunge lipitishe kile kinachoitwa mswaada wa matumizi kabla ya mashauriano juu ya masuala mengine kama vile kupunguza matumizi na program yake ya afya maarufu kama OBAMACARE. Warepublican wengi wanataka mashauriano kabla ya kupiga kura juu ya bajeti.
XS
SM
MD
LG