Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:45

Viongozi wa G7 wawasili Hiroshima kuzungumzia vikwazo vikali dhidi ya Russia


Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden.

Viongozi wa G-7 wamewasili Hiroshima, Japan Alhamisi ili kuzungumzia vikwazo vikali dhidi ya Russia na ulinzi kutokana na ushindani wa kiuchumi wa China wakiwa wamezunguukwa na kumbukumbu za gharama mbaya za vita.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amewapokea viongozi sita kutoka nchi zenye demokrasia imara mjini kake – mji ambao ulipata uharibifu wa Nyuklia na sasa umejaa makumbusho ya amani.

Kwa siku tatu viongozi akiwemo rais wa Marekani Joe Biden watajaribu kusukuma mbele mshikamano wa pamoja dhidi ya Russia, china, na maswala mengi muhimu ambapo maslahi ya washirika hayako sawa kila wakati.

Biden aliwasili Hiroshima kukiwa na mvua kubwa Alhamisi akiwa rais wa pili wa marekani baada ya Barack Obama kuzuru mji huo uliopigwa na kusambaratishwa na bomu la atomic la Marekani linalojulikana kama “ little Boy” . katika mkutano huo wa G-7 unaoanza Ijumaa , uvamizi wa russia wa miezi 15 sasa nchini Ukraine utakuwa ni agenda ya juu .

XS
SM
MD
LG