Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:04

Japan yaimarisha ulinzi wa mkutano wa G7 baada ya Waziri Mkuu kushambuliwa


Maandalizi ya Mkutano wa G7 nchini Japan.
Maandalizi ya Mkutano wa G7 nchini Japan.

Ulinzi ni mkali sana  katika  kila mkutano wa G7 lakini mwenyeji wa mwaka huu Japan ina  mengi zaidi ya kuthibitisha baada ya shambulizi la mwezi uliopita kwa Waziri Mkuu na mauaji ya mwaka 2022 ya Waziri Mkuu wa zamani Shinzo Abe.

Mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani aliyeuawa Shinzo Abe, Septemba 27, 2022.
Mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani aliyeuawa Shinzo Abe, Septemba 27, 2022.

Takriban maafisa wa usalama 24,000 watapelekwa Hiroshima wakati wa mkutano wengi wakitoka maeneo mengine ya nchi.

Kabla ya mazungumzo ya Mei 19 hadi 21 , polisi wa doria wamekuwa wakipita kati ya vikundi vya watalii katika bustani maarufu ya peace park iliyoko magharibi mwa mji huo.

Wafanyakazi wa usalama pia walikuwa wakipita kwenye eneo la mto ambao unapita kwenye maeneo kama vile Atomic Bomb Dome kwa kutumia helikopta.

Hatua zimechukuliwa nje ya mji ikiwemo ikiwemo mji mkuu wa Tokyo ambako kuna ujumbe wa onyo la kuwepo ulinzi mkali kwa ajili ya mkutano huo.

Miji mikubwa nchini Japan kwa ujumla haina mapipa ya taka katika maeneo ya umma lakini maafisa wa usalama wamekuwa wakifunga maeneo mengine yanayoweza kuwa na tishio.

XS
SM
MD
LG