Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:38

Viongozi wa G20 wameweka mikakati ya kukabiliana na uhaba wa chakula


G20 yakubaliana kudhibiti bei ya vyakula
G20 yakubaliana kudhibiti bei ya vyakula

Viongozi wa mataifa Tajiri sana 20 duniani G20, wanakutana Bali Indonesia kwa mazungumzo kuhusu uhaba wa chakula duniani na mfumuko wa bei za bidhaa.

Mkutano huo unafanyika wakati Indonesia inajaribu kuhakikisha kwamba tofauti kati ya mataifa hayo kuhusu vita vinavyoendelea Ukraine, havivurugi mkutano huo.

Uvamizi wa Russia nchini Ukraine umetawala majadiliano katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo, huku mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Russia akiondoka kwenye mkutano kwa hasira akilalamika kuhusu ukosoaji wenye upendeleo dhidi ya Russia.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen, amesema kwamba vita vya rais wa Russia Vladimir Putin dhidi ya Ukraine vinaendelea kusababisha athari katika nchi nyingine kote duniani.

Yellen amesema kwamba maafisa wa Russia hawastahili kuwa katika mkutano wa nchi kubwa 20 kiuchumi duniani.

“Marekani itaendelea kupinga vita vya Putin na mauaji yanayofanywa na wanajeshi wake. Jumuiya ya kimataifa inastahili kumwajibisha Putin kwa hasara ya kiuchumi na kusababisha janga la kibinadamu kutokana na vita hivi. Tangu kuanza kwa vita hivyo, wanajeshi wa Russia wameendela kusababisha uharibifu mkubwa sana usioweza kufikiriwa hasa mashariki mwa Ukraine.” Amesema waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen.

Maafisa wa Indonesia wameeleza kuhusu tofauti zilizopo kati ya nchi za magharibi na Russia namna ya kuandika maswala makuu waliokubaliana katika mkutano huo, hasa kuelezea hali ya uchumi duniani na namna inavyoathiriwa na vita vinavyoendelea Ukraine, na ambavyo Russia imetaja kama oparesheni maalum.

XS
SM
MD
LG