Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisherehekea makubaliano hayo, akisema EU ilikuwa inaonyesha uongozi na uwajibikaji katika kuiunga mkono Ukraine na wanajua “nini kiko hatarini.”
“Hii iko imara, kwa muda mrefu, ufadhili unaotabirika kwa Ukraine,” Michel alisema kupitia X, mtandao uliokuwa zamani Twitter.
Rais wa Ukraine alikaribisha kura hiyo ya pamoja, akisema “imethibitisha umoja imara wa EU.”
Msaada endelevu wa kifedha wa EU kwa Ukraine utaimarisha kwa muda mrefu uthabiti wa kiuchumi na kifedha, ambao bado ni muhimu kama ilivyo wa kijeshi na shinikizo la vikwazo dhidi ya Russia,” Zelenskyy alisema kupitia X.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema kupitishwa kwa msaada huo Alhamisi ni kinyume “na kauli zozote kuhusu madai kuwa ‘msaada umewachosha wafadhili au unapungua” kwa ajili ya Ukraine.
Forum