Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:46

Viongozi wa ECOWAS wakutana kutahmini vikwazo dhidi ya Mali na Burkina Faso


Viongozi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi wakutana Accra, Ghana.
Viongozi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi wakutana Accra, Ghana.

Viongozi wa Jumuia ya uchumi ya Afrika Magharibi wanakutana Accra, Ghana Jumapili kutahmini vikwazo walivyowekea nchi tatu zinazotawaliwa na wanajeshi katika kanda hiyo yernye kukumbwa na mapinguzi na ghasia.

Viongozi hao wanakutana kujaribu kupanga ratiba za kurudisha utawala wa kiraia kwa haraka iwezekanavyo nchini Mali, Burkina Faso, na Guinea.

Wakihofia kutokea mapinduzi zaidi viongozi wa ECOWAS wameiwekea Mali vikwazo vikali vya biashara na kiuchumi. lakini vikwazo vyepesi dhidi ya Burkina Faso na Guinea.

Wakati wa mkutano wao wa June 4, viongozi wa ECOWAS hawakuchukua hatua zezote dhidi ya mataifa hayo matatu.

Vikwazo hivyo vimeathiri vibaya sana nchi maskini ya Mali ambayo uchumi wake tayari ulikua unakabiliwa na matatizo kufaitia uasi wa karibu miaka kumi unaofwanywa na wapiganaji wakislamu.

Akiufungua mkutano wa Jumapili, Rais Nana Akufo-Addo, wa Ghana amesema jumuia hiyo yenye wanachama 15 inadhamira ya dhati kuzisaidia nchi hizo kurudi katika mfumo wa kidemokrasia, na viongozi watachukua hatua zinazostahiki baada ya kusikiliza ripoti juu ya maendeleo ya juhudi hizo.

Baada ya miezi ya mazungumzo magumu, viongozi wa Mali waliidhinisha siku ya Jumatano mpango wa kuitisha uchaguzi wa rais hapo Februari 2024. Uchaguzi huo utatanguliwa na kura ya maoni juu ya mswada wa katiba hapo March 2023 na uchaguzi wa bunge baadae mwaka huo wa 2023.

Mpatanishi wa ECOWAS kuhusiana na suala la Mali, rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Johnathan, alitembekea Mali wiki iliyopita na inaripotiwa kwamba amefanya maendeleo makubwa katika juhudi zake.


XS
SM
MD
LG