Viongozi wa dunia wanakutana kwenye Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mkutano wenye lengo la kupunguza umasikini uliokithiri na magonjwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mkutano huo wa siku tatu huko New York unahudhuriwa na maraisi na mawairi wakuu 140 ili kutathimini juhudi za malengo ya maendeleo ya millennia MDG’s yaliyowekwa mwaka 2000.

Juhudi hizo zina lengo la kupatikana maendeleo katika maeneo nane, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na janga kubwa la njaa, kupunguza vifo vya watoto wachanga, kuboresha afya ya uzazi na kuhakikisha kuwepo kwa elimu ya msingi kwa wote.
Katika ripoti iliyotolewa mapema mwaka huu, Umoja wa Mataifa umeelza kwamba bila ya juhudi zaidi baadhi ya malengo hayo huwenda hayatafikiwa katika nchi nyingi.
Mzozo wa kiuchumi umeathiri sana juhudi za kuchangisha fedha, lakini katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon anasema hali yakutotabirika ya uchumi haiwezi kua kizingizio cha kupunguza juhudi za maendeleo.
Umoja wa Mataifa umesema unatarajia mkutano huo kumalizika kwa kutoa mpango wa kuleta maendeleo katika malengo yote nane ifikapo mwaka 2015.