Viongozi hao walikamatwa wakati wakishinikiza uhuru wa eneo hilo la Catalonia.
Hata hivyo kiongozi wa Catalonia aliyeondolewa madarakani na ambaye amekuwa mjini Brussels Ubelgiji kwa wiki moja sasa, Carles Puigdemont, hakuwa mahakamani.
Puigdemont amedai mashitaka hayo yamechochewa kisiasa na kwamba angerudi Uhispania baada ya kuhakikishiwa kuwa sheria haitakuwa na upendeleo kwa upande wowote.
Msemaji wa chama tawala cha Uhispania cha Popular ameambia shirika la habari la AP kuwa suala la Puigdemont kutojisalimisha mahakamani mjini Madrid huenda likapelekea kutolewa kwa hati ya kukamatawa pamoja na ombi la kurudishwa kwake nchini Spain.