Mkutano huo wa siku tatu vile vile unaangazia mfumo wa afya wa kanda hiyo, kupatikana kwa chakula, hali ya hewa, biashara na maswala ya usalama.
Mkutano huo ulianza Jumatano usiku, kwa waziri mkuu mkuu wa Bahamas Philip Davis kufungua kikao hicho cha nchi wanachama 15.
Davis na viongozi wengine wa Bahamas wameelezea wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wahamiaji kutoka Haiti, ambao wanasema wanabana sana bajeti ya visiwa hivyo vidogo.
Idadi kubwa ya wakimbizi hao wanakimbia hali mbaya ya maisha, umaskini, kuongezeka kwa ghasia, utekaji nyara na idadi ya magenge yenye nguvu sana kuongezeka baada ya kuuawa kwa rais Jovenel Moise.
Katibu Mkuu wa muungano wa viongozi wa Caribbean, Carla Barnett, amesema kwamba Haiti inahitaji msaada wa haraka kukabiliana na hali mbaya ya kibinadamu.
Waziri Mkuu wa Haiti ameomba msaada wa wanajeshi wa nje, lakini Umoja wa Mataifa haujachukua hatua kuhusiana na ombi lake.