Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:20

Viongozi wa Afrika Mashariki wakutana Burundi kujadili mzozo wa DRC


East African Community headquarters in Arusha, Tanzania.
East African Community headquarters in Arusha, Tanzania.

Viongozi wa Afrika Mashariki walikuwa nchini Burundi siku ya Jumamosi kwa ajili ya mkutano wa kanda kujadili mzozo unaoendelea mashariki mwa (DRC).

Mazungumzo hayo yalifanyika katika kitovu cha uchumi cha Burundi mjini Bujumbura na Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo ni juhudi za upatanishi ili kumaliza mapigano yanayozuka tena mashariki mwa taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati.

Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye anashutumiwa kuunga mkono makundi ya waasi mashariki mwa DRC, ni miongoni mwa wanaohudhuria kikao hicho, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini Burundi tangu mwaka 2011.

Mkutano huo wa viongozi unafanyika siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa kimkakati wa Kitshanga kufuatia mapigano makali ya siku kadhaa.

Vikosi vya DRC viliondoka Kitshanga Januari 27 katika kile makamanda wake walichokitaja kama mbinu ya kuwalinda raia.

Viongozi wa jumuiya hiyo yenye wanachama saba wanakutana wakati ambapo uhusiano kati ya Rwanda na DRC mwanachama wake mpya zaidi, umedorora sana.

Mataifa hayo mawili yamekuwa yakilaumiwa kuhusu hali ya usalama nchini DRC huku Kinshasa ikimtuhumu Rais Paul Kagame kwa kufadhili harakati za M23.

Kigali imejibu mapigo ikiishutumu DRC kwa kukiuka uadilifu wa ardhi yake ikitaja uvamizi mara nyingi katika anga yake kwa ndege za jeshi la DRC.

Katika hatua ya hivi karibuni maafisa watatu wa jeshi la Rwanda walifukuzwa kutoka Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Peter Mathuki aliiandikia Kinshasa Februari mosi akitaka majibu kuhusu kufukuzwa kwa maafisa hao watatu ambao walikuwa sehemu ya jeshi la kikanda.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imepokea kwa wasiwasi tarehe 30 Januari, 2023 kuhusu kufukuzwa kwa maafisa hao watatu waliotumwa na Jamhuri ya Rwanda katika Makao Makuu ya Kikosi cha Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Goma hadi Rwanda,” Mathuki aliandika katika barua aliyoituma kwa Rais Felix Tshisekedi.

“Mheshimiwa, unaweza kukumbuka kuwa kupelekwa kwa maofisa hao katika Makao Makuu ya Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki Kanda ya Goma kusaidia Kituo cha Uongozi wa Kanda ilikuwa ni uamuzi wa Wakuu wa Nchi katika kikao chao cha Mchakato wa Amani Mashariki mwa DRC,” alisisitiza.

Jumuiya ya Afrika Mashariki iliidhinisha kutumwa kwa kikosi cha ulinzi DRC mapema mwaka 2022. Kenya ilipeleka wanajeshi wake mwezi Novemba pamoja na Nchi Washirika wengine zikiwemo Uganda, Burundi, Rwanda, Sudan Kusini na Tanzania.

Kikosi hicho kimekuwa kikifanya kazi pamoja na mchakato wa upatanishi unaoongozwa na Jumuiya ya Afrika mashariki uliowezeshwa na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Mazungumzo bado hayajazaa matunda.

XS
SM
MD
LG