Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 00:03

Viongozi wa Afrika Magharibi wapanga mkutano  utakaofanyika Alhamisi kujadili hatua ya serikali ya Niger

Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Balozi Abdel-Fatau Musah (kushoto) na Mkuu wa Majeshi wa Nigeria, Jenerali Christopher Musa (Kulia) wakihutubia Wakuu wa Majeshi wengine wa ECOWAS Agosti 2, 2023. AFP

Umoja huo haujajibu moja kwa moja lakini ulisema Jumatatu utafanya mkutano wa Alhamisi kujadili mkwamo huo.

Viongozi wa Afrika Magharibi Jumatatu walipanga mkutano utakaofanyika Alhamisi kujadili hatua ya serikali ya Niger kukataa amri ya kumrejesha madarakani rais aliyeondolewa mamlakani na hivyo kuibua matumaini ya kimataifa ya kutafuta suluhu bila ya kutumia nguvu.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilikuwa imewaambia viongozi wa mapinduzi ya Julai 26 kujiuzulu ifikapo Jumapili la sivyo wakabiliwe na uwezekano wa uingiliaji wa kijeshi lakini utawala wa kijeshi badala yake ulifunga anga ya Niger na kuahidi kuilinda nchi hiyo.

Umoja huo haujajibu moja kwa moja lakini ulisema Jumatatu utafanya mkutano wa Alhamisi kujadili mkwamo huo uamuzi ambao Umoja wa Ulaya na Marekani zilisema unaruhusu nafasi ya upatanishi.

Akiba ya uranium na mafuta ya Niger na jukumu lake kuu katika vita na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la Sahel vinaipa umuhimu wa kiuchumi na kimkakati kwa Marekani, Ulaya, China na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG