Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:12

Viongozi Afrika magharibi wataka kuiwekea vikwazo Mali


Wanajeshi wanaotawala Mali wakiwa wanalinda makao makuu yao.
Wanajeshi wanaotawala Mali wakiwa wanalinda makao makuu yao.

Viongozi waECOWAS wanakutana huko Senegal ili kuangalia uwezekano wa kuiwekea vikwazo Mali.

Viongozi wa Afrika magharibi wanakutana Jumatatu ili kuzungumzia uwezekano wa kuiwekea vikwazo Mali ambapo viongozi wa mapinduzi wameahidi kurudisha utawala wa kiraia lakini wamebaki madarakani.

Viongozi kutoka jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS wanatarajia kukutana Senegal kufuatia kumalizika kwa saa 72 kwa uongozi huo wa kijeshi kurudisha demokrasia.

Jumapili kiongozi wa mapinduzi Kapteni Amadou Sanogo alisema katiba na taasisi zote za kiserikali zimerudishwa lakini hakutoa wakati maalum kwa uchaguzi.

Remi Ajibewa mkuu wa masuala ya kisiasa na uhusiano wa kimataifa wa ECOWAS aliiambia VOA ni hatua ya makusudi na iliyopangwa.

XS
SM
MD
LG