Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 09:32

Mshukiwa ugaidi wa Ubelgiji hakuwa na bomu


Afisa wa Ubelgiji amesema mkanda iliodhaniwa kuwa wenye vilipuzi huku ukiwa umejazwa chumvi na biskuti umepatikana kwenye mshukiwa aliyekamatwa wakati wa operesheni dhidi ya ugaidi mjini Brussels Jumatatu.

Mshukiwa huyo alikuwa amezua hali ya taharuki kuwa ana bomu kwenye eneo la maduka katikati mwa mji huo mkuu wa Ubelgiji saa kumi na moja za asubuhi.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa Waziri Mkuu, Charles Michael, ameitisha mkutano wa dharura asubuhi ya leo.

Eneo hilo la maduka lilifungwa baada ya tishio hilo huku wote waliokuwemo wakifanyiwa ukaguzi wa kiusalama.

Ubelgiji imekuwa katika hali ya tahadhari tangu shambulizi la Machi kwenye uwanja wa ndege na kituo cha treni mjini Brussels ambalo liliuwa watu 32.

XS
SM
MD
LG