Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 07:14

Vikosi vya waasi vimefanya shambulizi jipya nchini Ethiopia


Mapigano mapya yameibuka katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia

Hapo Novemba nne Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed alizindua operesheni ya kijeshi katika mkoa huu wa kaskazini mwa nchi ili kuwanyang’anya silaha na kuzikamata mamlaka za kieneo zilizopinga kutoka Tigray People’s Liberation Front (TPLF)

Vikosi vya waasi vimefanya shambulizi jipya katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia msemaji wa waasi aliliambia shirika la Habari la AFP Jumanne wiki mbili baada ya shambulizi la kwanza ambalo lilipelekea serikali kutangaza usitishaji mapigano.

“Jana tulifanya shambulizi kwenye mkoa wa Raya, kusini mwa Tigray, na tulifanikiwa kuondoa vikosi vya ulinzi vya serikali kuu na vikosi vya Amhara", Getachew Reda aliiambia AFP kwa njia ya simu.

Getachew pia alisema wapiganaji wa waasi bado wanavifuatilia vikosi vinavyoiunga mkono serikali leo siku ya Jumanne. Msemaji wa jeshi la serikali kuu hakuweza kupatikana mara moja na ilikuwa vigumu kuthibitisha madai ya Getachew kwa kuwa mitandao ya mawasiliano ilikatwa kabisa katika mkoa huo.

Hapo Novemba nne Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed alizindua operesheni ya kijeshi katika mkoa huu wa kaskazini mwa nchi ili kuwanyang’anya silaha na kuzikamata mamlaka za kieneo zilizopinga kutoka Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

XS
SM
MD
LG