Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema vikosi vya nchi yake vimeua wanamgambo 3,000 wa kundi la Islamic State nchini Syria na Iraq akihimiza kuwa hakuna taifa lingine lililofanya juhudi kiasi hicho katika kukabuliana na magaidi.
Akihutubia wakuu wa kijeshi kutoka mataifa ya Balkan mapema leo, Erdogan amewakemea wanaodai kuwa Uturuki inaunga mkono Islamic State.
Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO ilijivuta katika kujiunga na muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya Islamic State huku ikifokewa kwa kutofanya vya kutosha kulinda mipaka yake dhidi ya wapiganaji wanaoingia Ulaya.
Hata hivyo, Uturuki imesema kuwa inahitaji msaada zaidi kutoka mataifa ya magharibi hasa kwenye mpaka wa Syria ambapo eneo lake limekuwa kilikilengwa kwa mashambulizi ya roketi.