Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:37

Jeshi la Syria kushambulia ngome za IS


Mpiganaji wa kujitolea katika jeshi la serikali ya Syria akiwa amekaa juu ya kifaru katika jimbo la Raqqa.
Mpiganaji wa kujitolea katika jeshi la serikali ya Syria akiwa amekaa juu ya kifaru katika jimbo la Raqqa.

Jeshi la Syria linapanga kufanya mashambulizi huko Deir Ez-Zor na Raqqa, ngome mbili za Islamic State kaskazini-mashariki mwa nchi, kwa msaada wa jeshi la anga la Russia, amesema leo Ijumaa, Alexei Borodavkin, Balozi wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa huko Geneva.

Borodavkin, ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu kwenye taasisi nyingine za kimataifa huko Geneva, alisema jeshi limefanikiwa kupambana na IS na makundi mengine ya kigaidi, kama al-Nusra Front katika siku za nyuma na kuna matumaini ya kuendeleza juhudi hizo.

Kulingana na azimio 2254 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, utawala wa kusitisha mapigano nchini Syria hauwahusu Daesh, al-Nusra Front na makundi mengine ya kigaidi, ikiwa ni matokeo ya operesheni zinazofanywa na vikosi vya jeshi la Syria kwa kusaidiwa na vikosi vya anga vya Russia. mji wa Palmyra umekombolewa, na operesheni za mashambulizi zaidi zinapangwa kuekelezwa Deir Ez-Zor na Raqqa, Borodavkin amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Russia.

XS
SM
MD
LG