Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:38

Vikosi vya usalama vyashika doria Khartoum

Watu waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa kijeshi mjini Khartoum, Sudan, Alhamisi, Dec. 30, 2021.
Watu waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa kijeshi mjini Khartoum, Sudan, Alhamisi, Dec. 30, 2021.

Vikosi vya usalama vimeendelea kushika doria katika maeneo mbalimbali mjini Khartoum na miji Jirani, kwa mujibu wa mashahidi walizungumza na shirika la Habari la AFP.

Vikosi vya usalama vimeendelea kushika doria katika maeneo mbalimbali mjini Khartoum na miji Jirani, kwa mujibu wa mashahidi walizungumza na shirika la Habari la AFP.

Hayo yanajiri wakati maandamano makubwa yaliyopangwa dhidi ya utawala wa kijeshi yakitarajiwa kufanyika Jumanne. Hali kadhalika hatua hiyo ya maafisa wa usalama kutumwa mitaani inajiri siku mbili tu baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok kujiuzulu.

Mashahidi wamesema kwamba barabara zinazoelekea makao makuu ya jeshi mjini Khartoum zimefungwa, huku polisi wengi wa kupambana na machafuko, na wanajeshi wakishika doria.

Wanaharakati wanaopigania demokrasia nchini humo wamezidisha shinikizo tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Oktoba 25, na kuongozwa na mkuu wa majeshi jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye pia alimweka kizuizini waziri mkuu na baadhi ya mawaziri.Waandaaji wa maandamano wamewahimiza waandamanaji kujitokeza kwa wingi na waandamane hadi katika ikulu ya rais mjini Khartoum, hadi pale watakapopata ushindi.

XS
SM
MD
LG