Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:26

Vikosi vya usalama vyafyatua risasi kutawanya watu Syria


Wafuasi wa Rais Bashar al-Assad wa Syria wakiandamana katika mji wa kaskazini wa Aleppo, March 27, 2011
Wafuasi wa Rais Bashar al-Assad wa Syria wakiandamana katika mji wa kaskazini wa Aleppo, March 27, 2011

Mashahidi wanasema vikosi vya usalama vya Syria vimefyatua risasi hewani kutawanya maandamano ya wanaharakati


Mashahidi wanasema vikosi vya usalama vya Syria vimefyatua risasi hewani kutawanya maandamano ya wanaharakati wa upinzani kusini mwa mji wa Daraa.

Mashahidi wa wanasema mamia ya waandamanaji wanaoipinga serikali waliokusanyika jumatatu katika mji wa Daraa kabla ya vikosi vya usalama kufyatua risasi na gesi ya machozi.

Hata hivyo hakukuwa na taarifa za majeruhi .

Maandamano ya kuipinga serikali yaliongezeka ijumaa iliyopita kutoka Daraa mpaka miji mingine ya Syria ikiwemo ule mji wa bandari wa Latakia na mji mkuu, Damascus.

Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake Marekani –Human Rights Watch, limesema takriban watu 61 wamekufa tangu kuzuka kwa ghasia hizo upande wa kusini Machi 18.

Daraa imekuwa ni kituo muhimu cha maandamano yaliyochukua zaidi ya wiki moja kupinga serikali ya rais Bashar Assad.

XS
SM
MD
LG