Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:51

Vikosi vya usalama vya Israel, vimempata na kumuua mshukiwa wa mauaji ya watu wawili

Mazishi ya afisa usalama wa Israel.
Mazishi ya afisa usalama wa Israel.

Baada ya msako uliotumia saa kadhaa, vikosi vya usalama vya Israel, Ijumaa vimesema kwamba vimempata na kumuua mshukiwa wa mauaji ya watu wawili, na kujeruhi wengine kadhaa baada ya kufyatua risasi katika klabu ya pombe jana Alhamisi mjini Tel Aviv.

Mamlaka zinazo husika zinasema mtu huyo alikutwa karibu na msikiti katika kitongoji cha Jaffa. Shin Bet, idara ya Israel ya usalama, imemtambulisha mtu huyo kuwa ni mkazi wa eneo la Jenin kutoka ukanda wa Gaza mwenye umri wa miaka 28.

Picha za shambulizi hilo kutoka eneo la tukio zimeonyesha polisi wakiwasili, na kuelekeza bunduki zao katika sehemu za juu za jengo pamoja na mlipuko. Saa kadhaa baada ya kufyatua risasi hakukuwa na taarifa kamili, hata hivyo wasiwasi umekuwa ukiongezeka nchini Israel baada ya wimbi la matukio kama hayo yanayofanywa na Wapalestina kuua watu 11.

XS
SM
MD
LG