Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:17

Vikosi vya Syria vyasonga mbele karibu na Palmyra

Maafisa wa eneo hilo na kundi la Uingereza linalo angalia vitendo vya haki za binadamu vinasema vikosi vya serikali vimefunga kuingia na kutoka katika upande wa kusini na magharibi mwa mji wa Palmyra.

Vikosi vya Syria vinavyosaidiwa na mashambulizi ya anga ya Russia vimesonga mbele nje kidogo ya mji wa kale wa Palmyra katika kampeni yake ya kukomboa eneo la wanamgambo wa Islamic State.

Maafisa wa eneo hilo na kundi la Uingereza linalo angalia vitendo vya haki za binadamu vinasema vikosi vya serikali vimefunga kuingia na kutoka katika upande wa kusini na magharibi mwa mji wa Palmyra.

Kundi la Islamic State lilikamata eneo hilo mwezi Mei mwaka 2015 na kuonyesha ishara ya kuwepo mara baada ya wapiganaji wake kubomoa kituo cha kale cha kumbukumbu cha Kiroma ambacho kinatambuliwa na idara ya Umoja wa Mataifa ya UNESCO kwamba ni eneo la urithi wa dunia.

XS
SM
MD
LG