Wizara ya Ulinzi ya Russia Jumatatu ilitoa ripoti ya mapigano ikisema kuwa jeshi la Russia lilivamia majengo ya ulinzi ya Ukraine kwa kutumia silaha zake za kulenga shabaha, ili kurudisha nyuma mashambulizi ya kijeshi ya Ukraine.
Operesheni hii iko katika maeneo mbalimbali ikiwemo Donetsk, Kupiansk na Kherson na pia kuvamia kituo chake cha udhibiti cha mfumo wa ndege zisizo na rubani UAV, ghala la silaha na malengo mengine.
Jeshi la anga la Russia limesema pia lilizuia mashambulizi ya roketi kadhaa na ndege zisizokuwa na rubani za jeshi la Ukraine.
Siku hiyo hiyo, mkuu wa majeshi ya Ukraine pia alitoa taarifa juu ya maendeleo ya mapigano akisema kuwa katika saa 24 zilizopita jeshi la ukraine limeendelea kupigana katika maeneo mbalimbali na jeshi la Russia katika ukingo wa mto Dnieper na maeneo mengine.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.
Forum