Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:23

Rais wa Afghanistan akubali mpango wa Obama


Vikosi vya Marekani, Kabul, Afghanistan, May 17, 2015.
Vikosi vya Marekani, Kabul, Afghanistan, May 17, 2015.

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, leo ameukaribisha mpango wa Rais wa Marekani Barack Obama wa kuendelea kubakisha vikosi vya jeshi 8,400 nchini Afghanistan mpaka mwisho wa utawala wake.

Ghani amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa majeshi hayo nchini Afghanistan ni ishara ya ushirikiano bora unaoendelea kati ya mataifa hayo mawili katika jitihada za kupambana na madui mmoja na kuimarisha usala katika eneo hilo.

Hata hivyo, wataalam wanasema kuwa hatua hiyo ya Obama inayacha maswali mengi yasiojibiwa kuhusu mwelekeo wa kuchukua katika siku zijazo, huku hali ya usalama ikizidi kuzorota.

Utawala wa Obama mwanzo ulipanga kupunguza idadi ya vikosi vya Marekani kutoka 9800 kufikia 5,500 ifikapo mwishoni mwa 2016.

Lakini Obama alitangaza Jumatano kwamba hali ya usalama Afghanistan inaendelea kuwa mbaya na kwa hiyo anaacha vikosi vingi zaidi kuliko alivyopanga hapo awali mpaka mwisho wa utawala wake ambao utakamilika Januari 20, 2017.

XS
SM
MD
LG