Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:31

Wapiganaji wa Machar waripotiwa kuingia DRC


Vikosi vinavyomtii Makamu Rais wa kwanza wa zamani Sudan Kusini, Riek Machar.
Vikosi vinavyomtii Makamu Rais wa kwanza wa zamani Sudan Kusini, Riek Machar.

Wapiganaji wa Makamu Rais wa kwanza wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar, hivi sasa wanaripotiwa kuwepo huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya congo-DRC wakikaribia kwenda maeneo ya Sudan Kusini mahala ambapo kundi la upinzani la Sudan People’s Liberation Army, SPLM-IO linadhibiti anasema msemaji wa Machar, James Gadet Dak.

Hatua hii inafuatia mzozo wa kijeshi katika mji mkuu Juba huko Sudan Kusini kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vya upinzani vya Makamu Rais wake wa kwanza wa zamani, Riek Machar.

Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar
Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar

Matamshi ya Dak yamekuja baada ya serikali mjini Kinshasa kuelezea wasi wasi wa usalama kwenye eneo lake ikiripotiwa kukiambia kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC-MONUSCO kuwaondoa kutoka kwenye eneo lake kiasi cha wanajeshi 750 wanaomtii Machar.

Vikosi hivyo vinavyomlinda Machar ambaye alikatiza DRC mahala ambako aliokolewa na kupatiwa huduma ya madawa na ofisi za Umoja wa Mataifa. Hivi sasa yupo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum lakini wanajeshi wake ambao wameweka silaha chini, bado wapo nchini DRC.

XS
SM
MD
LG