Wakati matumaini ya kupata mafanikio katika mazungumzo wiki hii huko Misri yamefifia yakilenga mahasimu wanaopigana Israel na wanamgambo wa Hamas kufikia makubaliano ya sitisho jipya, huku mashambulizi ya anga, mashambulizi ya mabomu na mapigano yameripotiwa katika makazi ya palestina.
Leo jeshi la Israel limeamuru wakaazi wa Al- Bureij katikati mwa Gaza kuhamia kusini haraka ikiashiria lengo jipya la mashambulizi ya ardhini ambayo tayari yameliharibu eneo la kaskazini mwa ukanda huo na kusababisha uvamizi mkubwa upande wa kusini.
Serikali ya Israel chini ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu imeapa kulitokomeza kundi la Hamas , kundi la kiislamu linaloongoza Gaza baada ya wapiganaji wake kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka Octoba 7 na kusababisha vifo vya watu 1,200 na kuwashikilia mateka watu 240 kwa mujibu wa hesabu za Israel.
Lakini idadi kubwa ya vifo wakati wa kampeni za kijeshi za Israel za kujibu mashambulizi zimeongeza ukosoaji mkubwa hata kwa Mshirika mkuu Marekani.
Vyanzo vya habari hii ni mashirika mbalimbali ya habari.
Forum