Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:22

Vikosi vya Iraq vyasonga mbele


Muungano wa vikosi vya Iraq, vinasonga mbele wakiwa katika siku ya tatu ya vita kuelekea Tikrit, huku wakikabiliwa na walenga shabaha wa Islamic State, na mabomu yaliyotegwa barabaran.

Shababa yao kuu ni kuiteka ngome hiyo ya kijeshi ya kundi hilo lenya siasa kali kaskazini mwa mji mkuu wa Baghdad.

Inakadiriwa wapiganaji 30,000 wanasonga mbele kuelekea mji huo unaoshikiliwa na kundi hilo, ikichukuliwa ni uvamizi mkubwa kabisa wa Iraq mpaka sasa.

Hizo ni juhudi za kuchukua tena udhibiti wa ardhi zilizochukuliwa na wanamgambo wa Islamic State toka mwaka jana.

Kundi hilo hapo Jumanne limedai raia wa Marekani aliyejulikana kana Abu Dawul Al-Amriki alifanya shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya vikosi vya Iraq, vinavyopambana nao karibu na mji wa Samarra, kituo ambacho vikosi vya Islamic State vilianza uvamizi wao wa Tikrit.

Madai ya Islamic State bado hayajathibitishwa.

XS
SM
MD
LG