Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 11:17

Vijana waliokufa kwenye klabu wazikwa Afrika kusini


Rais wa Afrika kusini akiwa kwenye mazishi ya vijana waliokufa kwenye klabu.
Rais wa Afrika kusini akiwa kwenye mazishi ya vijana waliokufa kwenye klabu.

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa Jumatano wakati akihudhuria mazishi ya vijana 21 waliofariki kutokana na mkasa kwenye klabu moja cha usiku takriban wiki mbili zilizopita amesema kwamba ni lazima maafisa wachukue hatua za kuzuia uuzaji wa pombe kwa vijana walio na umri wa chini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Ramaphosa amesema kwamba, " Huenda tusifahamu hasa kilichotokea, lakini tunachofahamu ni kwamba sheria ilivunjwa usiku huo, na labda mara kadhaa hapo kabla." Mazishi hayo yanasemekana kuhudhuriwa na zaidi ya waombolezaji 1,000 kwenye mji wa East London wakati majeneza yakipangwa katika mistari miwili.

Ramaphosa amehudhuria mazishi hayo wakati taifa lake linapokabiliana na changamoto kadhaa zikiwemo kukatika kwa huduma za umeme, madai ya ufisadi pamoja na uchunguzi unaoendelea wa fedha nyingi zilizopatikana zikiwa zimefichwa kwenye nyumba moja kwenye shamba lake.

XS
SM
MD
LG