Mashariki mwa Congo kumekuwa na migogoro kwa miaka mingi, ambapo kundi maalufu la M23 ni miongoni mwa zaidi ya makundi 100 yenye silaha yakipigania kijikita katika eneo hilo lenye utajiri wa madini jirani na mpaka wa Rwanda.
Baadhi wamekuwa wakishutumu kufanyika kwa mauaji ya watu wengi.
Kukiwa na waasi wa M23 darzen chache za kilometa kutoka Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, walinda amani wakiwa na MONUSCO, shirila la Umoja wa Mataifa linalohusika na usalama huko DRC wamekuwa wakifanya doria katika mitaa ya DRC kwa miguu.
Brigadia Jenerali Ranjan Mahajan wa Monusco, kamanda wa sekta ya kituo cha Kivu Kaskazini, ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa watu wake wamekuwa wakifanya marekebisho ya mkakati wao kulingana na tishio.
Hali ya usalama inatisha, kuliwa na mapigano ya mara kwa mara, mauaji ya raia na watu wengi kupoteza makazi.
Kulingana na takwimu za UNHCR, watu wapatao 521,000 wamepoteza makazi huko Goma na kutawanyika katika maeneo mbalimbali ya Kivu Kaskazini.
Idadi ya 233,000 wako katika makazi yasiyo rasmi.
Wakikabiliwa na hali hii, vijana wengi utoka maeneo tofauti wamekuwa wakijiorodhesha katika kundi lenye silaha linaloitwa the patriot au Wazalendo kwa Kiswahili.
Forum