Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 07:16

Vijana watumia muziki kuhamasisha amani Kenya


Vijana wa kundi
Vijana wa kundi

Wakati huu ambapo taifa la Kenya linatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu mwezi Agosti mwaka huu, juhudi mbalimbali za kuhimiza amani zinaendelea nchini humo.

Miongoni mwa watu wanaolengwa zaidi katika kampeni ni vijana ambao mara nyingi wao ndio wanaohusishwa na vurugu wakati na hata baada ya uchaguzi.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya VOA, Salma Muhamed amesema kundi moja la vijana wasanii mjini Mombasa linalojulikana kama 'Neon The Band' tayari wameanza kuchukua jukumu hilo wakitunga nyimbo zenye ujumbe wa amani na kuhimiza vijana wengine kujitahidi katika kazi zao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:21 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

“Bendi yetu ina asili ya kiafrika, tunatumia ala za muziki kama vile gitaa na ngoma na nyimbo zetu zina ladha tofauti,” anasema Pascal, mshiriki wa kundi hilo.

Kundi la 'Neon The Band' linahusisha vijana wanne, na washiriki wa kundi hilo wanatoka katika jamii tofauti nchini Kenya.

Wao ni waathirika wa moja kwa moja wa vurugu za uchaguzi za mwaka 2007 zilizotokea nchini Kenya.

Wanasema walishuhudia mauaji ambapo marafiki zao waliuwawa kwa kupigwa risasi, jambo lililowafanya kuchukua hatua ya kuhamasisha vijana wenzao kuilinda amani kupitia burudani ya muziki.

Vijana nchini Kenya wamelaumiwa kwa kujihusisha na tabia zinazokiuka maadili kama vile kuzua vurugu na kupora mali ya umma, hasa wakati wa mikutano ya kisiasa.

Vile vile uhasama wa kikabila nchini Kenya umetajwa kama tishio kuu linalowagawanya vijana wengi.

Hata hivyo 'Neon The Band' inaamini kwamba muziki unaweza kubadilisha hali hiyo katika jamii kwani vijana wengi wanapenda kusikiza nyimbo.

“Sisi tunatumia muziki kama kifaa cha kufikisha ujumbe, tumechukua jukumu la kuongea kwa niaba ya yule ambaye hawezi kuzungumza katika jamii,” naongeza Kevin.

Kundi hili limekuwa likitumbuiza katika matamasha mbalimbali mjini Mombasa, na vile vile hujipatia kipato kutokana na matamasha hayo.

Ikizingatiwa kuwa huu ndio mwaka wa uchaguzi mkuu nchini Kenya, vijana hawa wanadai kuwa aghlabu wanasiasa ndio wanaowachochea vijana kuzua vurugu.

Hata hivyo wanasema kuwa wamefanikiwa kuwafikia vijana wengi kupitia nyimbo zao, na nia yao ni kuzunguka maeneo mengine nchini kuhamasisha vijana kabla uchaguzi mkuu.

Wakati wa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mwaka 2007 zaidi ya watu 1, 000 walipoteza maisha yao huku maelfu wakitoroka makwao.

Aidha uchaguzi uliofuata wa mwaka 2013 hali ilikuwa shwari, lakini bado iko haja ya kuendelea kueneza ujumbe wa amani na umoja kote nchini hivi sasa kabla uchaguzi wa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG