Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:22

Wamarekani wapanga kujiunga na Islamic State.


Kituo cha kiislamu katika jimbo la Mississippi ambapo Muhammad Dakhalla alikuwa mwanachama.
Kituo cha kiislamu katika jimbo la Mississippi ambapo Muhammad Dakhalla alikuwa mwanachama.

Vijana wawili wenye uhusiano wa kimapenzi wamekamatwa na kushitakiwa kwa kujaribu kujiunga na wanamgambo wa kundi la Islamic State huko Syria. Muhammad Dakhalla mwenye umri wa miaka 22 na mpenzi wake wa kike Jaelyn Young mwenye umri wa miaka 20 walikamatwa na maafisa wa FBI jumamosi baada ya kusafiri hadi uwanja wa ndege wa Golden Triangle ulioko Columbus, Mississippi wakiwa na kusudi la kupanda ndege wakielekea Amsterdam na hatimae Istanbul.

Wawili hao wameshitakiwa kwa kupanga njama na kijaribu kutoa vifaa vya kusaidia Islamic State. Kwenye taarifa ya kiapo iliotolewa na afisa wa FBI, wote wawili wamekiri mashitaka baada ya kukamatwa. Kulingana na waraka wa malalamishi, vijana hao wawili walizungumza kwa njia ya mitandao na mawakala wa FBI, kwamba walikusudia kusafiri hadi Syria kusaidia kundi la Islamic State.

XS
SM
MD
LG