Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:35

Vigogo wa siasa za Kenya wameanza kukiri kushindwa


Wanasiasa wa Kenya Moses Kuria (kulia) na aliyekuwa mbunge wa kiambu Ferdinand Waititu (Kushoto) walipofikishwa mahakamani Nairobi, kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi. June 14, 2016. PICHA: REUTERS
Wanasiasa wa Kenya Moses Kuria (kulia) na aliyekuwa mbunge wa kiambu Ferdinand Waititu (Kushoto) walipofikishwa mahakamani Nairobi, kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi. June 14, 2016. PICHA: REUTERS

Wanasiasa maarufu na wa muda mrefu nchini Kenya wameanza kukubali kushindwa hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa.

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema kwamba amekubali kushindwa katika kinyang’anyiro cha ugavana, kaunti ya Kiambu.

“Nimefurahia miaka 8 ya kuwa mbunge wenu, narudi katika kazi yangu binafsi.” Ameandika Kuria.

Mosea Kuria ni kiongozi wa chama cha Kazi ambacho kimemuunga mkono mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha UDA William Ruto.

Wagombea wa Ugavana katika kaunti ya Kiambu ni pamoja na seneta Kimani Wamatangi wa UDA, aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo William Kabogo wa chama cha Tujibebe, na mgombea huru Patrick 'WaJungle' Wainaina.

Kuria ni mkosoaji mkubwa sana wa rais Uhuru Kenyatta na mgombea wa urais Raila Odinga.

Wagombea wengine ni Juliet Kimemia, Mwende Gatabaki wa Safina na gavana wa sasa James Nyoro wa chama cha Jubilee.

Mbunge Naomi Shaban akubali kushindwa

Mbunge wa muda mrefu Naomi Shaban, wa eneo bunge la Taveta naye amekubali kushindwa.

Shaban ameiwakilisha Taveta kwa mihula minne. Amesema kwamba ameshindwa na Bwire Okano, wa chama cha Wiper, japo tume ya uchaguzi haijatangaza rasmi mshindi.

"Namtumia salamu za pongezi kwa mshindani wake Bwire. Ahsante watu wa Taveta kwa kunipa fursa ya kuwawakilisha kwa muda wa miaka 20” ameandika Shaban, ambaye pia ni naibu wa chama cha Jubilee chake rais Uhuru Kenyatta.

XS
SM
MD
LG