Wasiwasi, kuchanganyikiwa na upweke, vitu ambavyo wataalam wa afya wanasema vinaweza pelekea mtu kujiua, vinasemekana kuongezeka nchini Zimbabwe kutokana na hali ngumu ya kiuchumi ilioko.
Utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la Zimbabwe linalojulikana kama Varume Svinurai/ Vukani Madoda, unasema kuwa mwaka 2013 asilimia 55 ya vifo kutokana na kujiuwa nchini humo vilikuwa vya wanaume.
Idadi ya kujiuwa vile vile ilipanda kutoka aslimia 53 mwaka 2012 hadi 55 mwaka uliofuata.
Dkt Bonde kutoka taasisi ya Zimbabwe Wellness And Lifestyle, anasema ni lazima serikali ishughulikie maradhi haya yaliojificha akiongeza kuwa vituo vya afya nchini humo vinahitaji kuwa na vifaa ili kukabiliana na matatizo ya akili.