Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 08:19

Vifo kutokana na Malaria vyapungua duniani


Kampeni dhidi ya Malaria

Shirika la afya Duniani ( WHO) linaripoti kuwa kwa jumla idadi ya vifo kutokana na Malaria imepungua tangu mwaka wa 2000, na kwamba idadi ya watu wanaougua inaendelea kupungua.

Nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ndizo zinazolemewa zaidi na ugonjwa wa Malaria, zikiwa na asilimia 90 ya vifo vyote duniani vinavyotokana na ugonjwa huo.

Lakini ripoti ya mwaka huu ya Malaria Duniani inasema idadi ya watu barani Afrika imekuwa kwa asilimia 43 tangu mwaka wa 2000, huku idadi ndogo ya watu wakiambukizwa ugonjwa huo.

Meneja wa program ya WHO juu ya Malaria Duniani Pedro Alonso anasema idadi ya watu walioambukizwa ilishuka kutoka milioni 173 mwaka 2000 na kufikia milioni 128 mwaka 2013.

Anasema hizo ni habari njema haswa kwa watoto ambao ndiyo waathiriwa wakubwa wa ugonjwa huo hatari na ambao unaweza kuzuilika.

WHO inasema idadi hiyo imepungua kwa sababu watu sasa wana njia nyingi za kudhibiti Malaria, ikiwemo dawa za kuuwa mbu na nyavu za kujisitiri na mbu nyakati za kulala.

Na ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, shirika hilo litakuwa limetoa msaada wa nyavu za kuzuia mbu milioni 214 kwa nchi zinazoathiriwa sana na Malaria.

XS
SM
MD
LG