Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:32

Video ya polisi yaonyesha sababu ya kifo cha Mmarekani mweusi

waandamanaji katika matembezi ya kudai plisi watoe video itakayoonesha kifo cha mmarekani mweusi huko Charlotte, North Carolina
waandamanaji katika matembezi ya kudai plisi watoe video itakayoonesha kifo cha mmarekani mweusi huko Charlotte, North Carolina

Moja ya video inaonesha Scott akitoka nje ya gari lake na kugeuka upande wake wa kushoto akisimama kwenye eneo la kuegesha magari kwa kiasi cha sekunde tatu kabla ya kufyatuliwa risasi na anaonekana kuanguka chini.

Video iliyotolewa na polisi wa mji wa Charlotte katika jimbo la North Carolina, Marekani inaonesha majibizano yaliosababisha kifo kati ya polisi na Keith lamont Scott, mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 43 ambaye alifyatuliwa risasi na kuuwawa Jumanne iliyopita, tukio lililochochea ghasia katika mji huo mkubwa huko North Carolina.

Video hizo mbili kutoka kamera aliyovaa ofisa polisi na ile ya kutoka kwenye gari la maafisa inayorekodi matukio yote yanayoendelea zilitolewa jumamosi baada ya siku kadhaa za wito kutoka kwa waandamanaji kutaka watoa picha hizo hadharani.

Moja ya video inaonesha Scott akitoka nje ya gari lake na kugeuka upande wake wa kushoto akisimama kwenye eneo la kuegesha magari kwa kiasi cha sekunde tatu kabla ya kufyatuliwa risasi na anaonekana kuanguka chini.

Video ya pili haimuoneshi Scott kabla ya kuanguka. Sauti ya video hiyo imekatwa kwa sekunde 23 za kwanza. Siku ya tano ya maandamano dhidi ya ufyatuaji risasi yalikuwa ya Amani baada ya kutolewa video hizo.

Jumapili darzeni ya waandamanaji waliimba “maisha ya watu weusi yathaminiwe” nje ya uwanja wa mpira wa football, kati ya Carolina Panthers na Minnesota Vikings uliofanyika huko Charlotte.

XS
SM
MD
LG