Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:11

Wamachinga wapoteza mitaji kufuatia bomoabomoa machinga complex


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga jijini Dar es salaam, Tanzania wamekumbwa na taharuki baada ya kufika katika eneo lao la biashara nje ya jengo la machinga complex na kukuta vibanda vyao vimebomolewa.

Zoezi hilo limefanyika usiku wa kuamkia Jumatatu na kwa hasira wafanyabiashara hao wakachoma moto barabara kwa kutumia matairi na takataka nyingine.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa wafanyabiashara hao wamedai kuwa walipewa siku tatu kuhakikisha wanaondoa bidhaa zao.

Hata hivyo wamedai kuwa waliandika barua ya kuomba kusitishwa kwa zoezi hilo ili wapatiwe vizimba lakini cha kushangaza ni kwamba wamevunjiwa hata bila kupata majibu ya baraua yao.

Pia wamelalamika kupotea kwa bidhaa zao ambazo baadhi yake zimeibiwa na nyingine hawajui zimepelekwa wapi.

Mfanyabiashara wa machinga Complex Yohana William amelalamika kuwa mtaji wake wote umepotea kwani alikuwa ameaminiwa na mali za watu kufanya biashara lakini vunjavunja hii imemharibia biashara yake, na amepoteza kila kitu.

“Vibanda vyetu vimebomolewa, nimebakia hivihivi kama nilivyo unavyoona nina mkopo wa watu, walikuwa wananiamini kwenye kizimba tuko kikundi pamoja sasa tunashangaa…,” mfanyabiashara huyo amesema kwa masikitiko makubwa.

“Sasa tunashangaa rais ameruhusu wafanyabiashara kama sisi wako barabarani, lakini sisi wafanyabiashara wadogo tuliovumilia miaka yote, miaka sita tuko hapa, hili jengo linaitwa machinga complex sasa tumekuja wamachinga wenyewe tunatolewa. Na pale ambapo wananambia niende sijaelekezwa,” amesema William.

Wakinamama wajasiriamali katika soko hilo walilaumu zoezi hilo la kubomoa vibanda vyao vya biashara ambavyo ndio vilikuwa vinawapatia riziki zao.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Mariam Hassan amewauliza viongozi waliobomoa vibanda vyao wanataka wawe mahakaba na majambazi?

Mwandishi wetu ameripoti kuwa vibada vyao vinadaiwa kubomolewa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri wa nchi ofisi ya rais (TAMISEMI), George Simbachawene la kuwataka waingie ndani ya jengo badala ya kuweka vibanda nje ya jengo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Dina Chahali, Tanzania

XS
SM
MD
LG