Serikali ya Venezuela imeipa Marekani, wiki mbili kupunguza wafanyakazi wa ubalozi wake mjini Caracas kufikia 17, wakati hali ya kutoelewana baina yao ikizidi.
Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela, Delcy Rodriguez, ametoa tamko hilo katika mkuutano na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani, mjini Caracas.
Amesema ni juu ya Marekani kuamua kati ya wafanyakazi 100 nani wa kumrudisha nyumbani.
Hatua hiyo inafuatia madai ya Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, siku ya Jumamosi, kwa kile alichokiita ni njama dhidi ya serikali yake ya kisosholisti.
Bwana Maduro, ameiamrisha wizara ya mambo ya nje kupunguza idadi ya maafisa katika ubalozi wa Marekani, kutoka 100 hadi 17.
Vilevile ameweka masharti ya kupata kibali cha kuingia nchini Venezuela, kwa watalii wa Kimarekani.
Bwana Maduro amedai Venezuela imewashikilia majasusi wa Kimarekani, akiwemo mmoja aliyemwita rubani wa Kimarekani mwenye asili ya Ki-Latino.