“Papa alikuwa na usiku wa amani na anapumzika,” Vatican imesema katika taarifa. Papa Francis alipata shida Ijumaa wakati akiwa katika hospitali ya Gemelli ya Roma, ambapo amelazwa kwa wiki mbili zilizopita.
Vatican imesema “tukio la pekee la kupumua” lilisababisha Papa mwenye umri wa miaka 88 kuvuta matapishi yake ambayo yalihitaji uingizaji hewa kwa mitambo.
Papa Francis alikuwa na fahamu wakati wa kipindi chote na aliweza kushirikiana na kushiriki nyanja mbalimbali za matibabu yake.
Vatican imesema Papa bado anafahamu zote na mwenye mwelekeo mzuri.
Habari za matatizo ya Ijumaa zinafuatia siku tatu za ripoti za kuboreka kwa hali ya afya ya Papa Francis.
Forum