Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 02:27

Uwezekano wa shambulizi la kigaidi Addis Ababa


Mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa

Ubalozi huo unasema umepata habari kuwa kundi la wanamgambo wa Somalia al-Shabab linalenga kushambulia wilaya ya Bole iliyoko kusini mashariki ya mji huo.

Ubalozi wa Marekani nchini Ethiopia umeonya juu ya uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi katika eneo moja la mji mkuu wa Addis Ababa.

Ubalozi huo unasema umepata habari kuwa kundi la wanamgambo wa Somalia al-Shabab linalenga kushambulia wilaya ya Bole iliyoko kusini mashariki ya mji huo.

Taarifa kutoka ubalozi huo inasema eneo mahsusi linalolengwa kushambuliwa halijulikani, lakini inaonya watu kutokwenda kwenye mahoteli, majumba ya kuabudia na maduka makubwa ya wilaya hiyo ya Bole, hadi itakapotolewa taarifa kuwa ni salama kwa sababu kuna uwezekano mkubwa sana wa shambulizi la kigaidi kwenye maeneo hayo.

Taarifa hiyo pia inashauri raia wa Marekani kutoingia kwenye maeneo yenye umati mkubwa wa watu ambayo ni maarufu kwa Waethiopia na raia wa kigeni.

Ethiopia ni moja ya nchi ambazo zimechangia majeshi yake Somalia kupigana dhidi ya kundi hilo la al-Shabab.

XS
SM
MD
LG