Mifululizo ya uvamizi wa mashamba katika kaunti ya Laikipia nchini Kenya ni kielelezo cha mivutano kuelekea uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Jumanne Agosti nane ambapo watu wengi wana khofu huwenda ikazusha ghasia zaidi zenye kusababisha vifo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP zaidi ya mwaka mmoja mashamba na nyumba katika kaunti ya Laikipia yamekuwa yakivamiwa. Wavamizi kawaida ni watu wanaohama hama makazi wanasema wamelazika kuingia katika hali hiyo kutokana na ukame mbaya unaofurumusha mifugo yao kuingia kwenye mashamba makubwa yanayomilikiwa na watu binafsi.
Lakini wakulima wengi walisema wanaamini uvamizi wa ardhi unachochewa kisiasa. Walisema wanasiasa wengi wanawahamasisha mamia ya waangalizi wa mifugo na maelfu ya wakulima waliokoseshwa makazi wote weusi na weupe kuwasaidia kushinda uchaguzi katika eneo.