Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 05:42

Uturuki yamsihi Gadhafi aondoke madarakani.


Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan .
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan .

Waziri mkuu amtaka Bw. Gadhaffi lazima aachie madaraka ili kuzuia watu wa Libya kuteseka zaidi.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemsihi kiongozi wa Libya Moammar Gadhaffi kuachia madaraka na kuondoka nchini humo mara moja.

Bw. Erdogan alisema jumanne mjini Istanbul kwamba Bw. Gadhaffi amechagua machozi, damu na uharibifu huku akidharau wito wa mageuzi. Alisema Bw. Gadhaffi lazima aachie madaraka ili kuzuia watu wa Libya kuteseka zaidi.

Uturuki imekuwa mshirika mkubwa wa serikali ya Libya na walionyesha upinzani wao mwezi Machi dhidi ya vikwazo au uvamizi wa kijeshi katika nchi hiyo.

Uturuki ilisema jumatatu inawaondoa wafanyakazi wake kutoka kwenye ubalozi wake. Ilikuwa ni moja ya nchi chache zilizoacha ubalozi wake wazi. Umoja wa mataifa iliondoa wafanyakazi wake mjini Tripoli siku ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG